Kibiti: Polisi watumia helikopta kuzima vurugu!

OSOKONI

JF-Expert Member
Oct 20, 2011
10,965
5,336
VURUGU kubwa zilizowalazimisha Polisi kutumia helikopta kuzituliza, zilitokea jana baada ya baadhi ya wakazi wa Kata ya Kibiti kuvamia kituo kidogo cha jeshi hilo wakitaka kukichoma moto katika kile kilichoelezwa kuwa ni kutaka kulipiza kisasi cha mwenzao kukamatwa na polisi na kisha kupigwa hadi kufariki dunia juzi.

Katika vurugu hizo, wakazi hao wengi wao wakiwa ni vijana, walifunga Barabara ya Kilwa kwa zaidi ya saa tatu hivyo kukwamisha usafiri wa kwenda na kutoka mikoa ya Mtwara na Lindi.

Vurugu hizo hazikuishia hapo kwani vijana hao walivamia nyumba za askari wa kituo hicho na kisha kutoa vyombo na kuviharibu. Katika tukio hilo, nyumba moja ilichomwa moto.

Hali ilivyokuwa
Kamanda wa Operesheni Maalumu ya Jeshi la Polisi nchini, Saimon Sirro alisema katika tukio hilo, nyumba hiyo ya jeshi imeteketezwa kabisa kwa moto na vyumba vinne vya nyumba nyingine walizopanga askari wengine jirani vimevunjwa... “Vijana hao walikuwa wakiingia na kutoa vyombo na nguo za askari waliopanga humo na kuzichoma moto.”

Kamanda Sirro alisema vurugu hizo zilitokea baada ya kupatikana kwa taarifa za kifo cha Hamis Athumani (30), mkazi wa Kibiti katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amepelekwa kutibiwa majeraha ambayo kamanda huyo alisema marehemu alidai kuyapata baada ya kupigwa na askari waliomkamata alipojaribu kuwatoroka walipomkamata kwa tuhuma za kuhusika na dawa za kulevya.

Alisema kukamatwa kwake kulitokana na operesheni ya msako wa bangi na dawa za kulevya.

Akizungumzia tukio hilo, shuhuda mmoja wa tukio hilo ambaye hakutaka jina lake liandikwe alisema baada ya kipigo hicho, kijana huyo alilalamika maumivu na hivyo ndugu zake walifika kituoni hapo na kumpeleka Kituo cha Afya Mchukwi.

“Hali yake iliendelea kuwa mbaya na akapelekwa Muhimbili ambako alifariki dunia jana alfajiri,” alisema shuhuda huyo na kuengeza: “Taarifa hizo zilipofika kijijini, baadhi ya vijana walikusanyika na kuanza kuhamasishana na kuanza kuziba barabara kwa matairi na kuvamia nyumba za askari na kuchoma moto.”

Baada ya ghasia hizo kupamba moto, jeshi liliamua kutumia helikopta ambayo ilitua Kibiti saa 5.50 asubuhi ikiwa na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wakiongozwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ulrich Mathei.

Kamanda Sirro alisema watu 18 wamekamatwa kwa kuhusika na vurugu hizo.

Chanzo cha vurugu
Inadaiwa kuwa Jumanne saa tatu usiku, askari wa Kituo cha Polisi Kibiti walivamia kambi ya vijana wanaodaiwa kujishughulisha na biashara ya dawa za kulevya inayojulikana kwa jina la Kosovo iliyopo Mbebetini karibu kabisa na Sekondari ya Kibiti.

Askari hao ambao baadhi ya wakazi wa Kibiti wamewaeleza kuwa ni mashujaa kwa hatua yao ya kuthubutu kuvamia kambi hiyo ambayo inadaiwa kushindikana kwa muda mrefu kushughulikiwa na askari wa Kituo cha Polisi Kibiti, walikumbana na upinzani mkali wa vijana wapatao 30 wakipinga kukamatwa kwa kiongozi wao.

Inadaiwa kuwa baada ya kumkamata, walimshambulia kwa virungu lakini kutokana na upinzani mkali waliopata kutoka katika kundi hilo, walishindwa kuondoka naye lakini walimwacha akiwa mahututi.

Habari hizo zilieleza kuwa vijana hao walimchukua kiongozi wao na kumpeleka Mchukwi kwa matibabu kabla ya kumsafirisha kwenda Muhimbili ambako alifariki dunia.

Baada ya kupatikana kwa taarifa za msiba huo, baadhi ya wananchi wa Kibiti waliandamana saa 1.22 asubuhi hadi kituo cha Polisi ambako waliharibu pikipiki tatu za polisi. Walitawanywa baadaye kwa baruti na silaha za moto.

Baadaye, polisi kutoka Ikwiriri walifika na kudhibiti kundi kubwa la watu hao wapatao 120 kwa mabomu ya machozi.

Askari afariki
Askari wa Kikosi cha Kutuliza ghasia (FFU) H21 PC Domick, amefariki dunia na wenzake wanne kujeruhiwa vibaya, baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka Kibaha Pwani kuelekea Rufiji kutuliza vurugu hizo kupinduka katika eneo la Mkuranga.

MWANANCHI
 
Jamani imefikia sasa tusingize siasa kwenye maswala ya polisi kupambana na wahalifu.Sasa wewe umeambiwa wauza madawa ya kulevya halafu unasema nguvu ya umma au unataka mtoto wako athirike ndo upate uchungu

serikali haina nia ya dhati ya kupambana na biashara ya madawa ya kulevya! mbona wanakamata vidagaa tu na sio mapapa yaliyoko ndani ya serikali yenyewe? ile listi ya wauza unga aliyopewa Kikwete na marehemu Amina Chifupa ulishasikia imefanyiwa kazi? kimyaaa...
 
Haina haja ya kuanza kubishana hapa sion ajabu huyo muuza dawa kufa kama angetii sheria bila shuruti yote haya yasingekuwepo!! Tusiingize siasa kwenye haya mambo!!
 
Kwa siku za karibuni nimegundua kuwa mara nyingi vitendo vinavyo pelekea ugomvi mkubwa kati ya polisi na wananchi huwa ni mambo madogo sana ambayo yangeshughulikiwa kwa umakini/busara yangeisha bila hata kuhitaji kutmia nguvu.badala yake kunaingia ubabe na kutaka kutunishiana misuli na baadaye yanafika pabaya - unasikia raia kauwawa au askari. IGP jiulize ni ngapi kati ya vurugu zinazohusu polisi zingweza kuepukika kirahisi tu, kwa nini busara hazitumiki, je, tunakwenda wapi? hivi jeshi la polisi huwa lina muda wa kufanya tafakari? Nimeweka tafakari au nimseme nimeelemea kwa kuwaswali polisi katika hili kwa sababu tofauti na wananchi jeshi ni taasisi. wahenga wanasema 'it takes two to tangle' hivyo upande mmoja ukidhamiriwa kuepusha vurugu inawezekana.
 
Jamani imefikia sasa tusingize siasa kwenye maswala ya polisi kupambana na wahalifu.Sasa wewe umeambiwa wauza madawa ya kulevya halafu unasema nguvu ya umma au unataka mtoto wako athirike ndo upate uchungu
Unatakiwa utafakari katika level ya juu ndugu yangu. Purchasing power ya watu wa kibiti ni ndogo mno, hakuna mfanyabiashara wa madawa ya kulevya atakayetoa madawa dar kupeleka kibiti ni upotevu wa muda.
Polisi wa tanzania ni lazima wakubambike issue ili wao waonekane wako sahihi. Nadhani wewe hauishi bongo au hujawahi kukumbana na hao polisi wakati wanapolazimisha mazingira ya kupewa rushwa.
 
sasa sidhani kama serikali itaweza hii mbinu ya raia kuvamia makazi ya maaskari.
 
Mi naona sasa Serikali itafikia sehemu wataiona nguvu ya umma ni nuksi kwani hata hizo risasi na bomu wanazotumi haitatosha kuwazuia raia wasifanye wanachotaka!

Polisisiem msipokuwa makini mtajajuta sana!

nguvu ya uuma katika kuuza mihadarati?
 
Jamani imefikia sasa tusingize siasa kwenye maswala ya polisi kupambana na wahalifu.Sasa wewe umeambiwa wauza madawa ya kulevya halafu unasema nguvu ya umma au unataka mtoto wako athirike ndo upate uchungu

JF imevamiwa na maharamia wasioipenda Tanzania ijayo. Kwa mjibu wa report ya mwananchi, kundi hilo limeshindikana kwa muda mrefu, askari kwa kuipenda kazi yake ameamua kujitosa kuokoa maisha ya vija waliopotea/athirika kwa matumizi ya mihadarati, kundi hilo wanaamua kupambanza na askari, vipigo vinaanza, sasa kuna nguvu ya umma au ujambazi?

Ungeniambia sera mbovu za CCM ndizo zinazowagharimu askari na wananchi ningekuelewa kwani CCM inafaham wote wanaojihusisha na uuzaji wa madawa ya kulevya, lakini haiwataji na imebaki na majina kapuni, hapa ningekuelewa.
 
Hi thana ya polisi jamii ndiyo inayowaharibia polisi embu iweken pemben mfanyanye kaz watanzania bado hawajaelimika vyakutosha kama wenzetu wa majuu,ingekua nikipnd cha mahita haya yote yasingetokea mmezd siasa polisi
 
Matumizi ya nguvu kupita shepga ndo matokeo yake haya,sasa wananchi hawaogopi tena polisi, hawahofii tena mabomu ya machozi na maji ya kuwasha, hawaliamini tena jeshi la polisi, wamejenga uadui na polisi. Hii si salama kwa amani ya nchi hata kidogo
 
nguvu ya uuma katika kuuza mihadarati?

Una uhakika kwamba ni muuza mihadarati? Kibiti na biashara ya mihadarati wapi na wapi?
Polisi wanaweza kusema chochote katika kujitetea. Yani bado tu unawaamini policcm wanaobambikia watu kesi za uongo kila siku. Hujamsikia hata gam,ba Lowasa akiwalaani kwa kubambikia wananchi kesi za uongo?

Hata kama ni muuza mihadarati ndio polisi wamuue? Ndo sheria inavyowaelekeza? Watu wengine sijui mnatumia nini kufikiri!
 
Back
Top Bottom